Monday 1 September 2014

UVAAJE WA SKAFU KATIKA KUIPENDESHA NGUO NA MUONEKANO WAKO



SEPTEMBER, 2014


Description: scarfs


Skafu ni urembo unaoweza kuvaliwa na aina yoyote ya nguo iwe ni vazi la kawaida au suti ya aina yoyote. Skafu inawezesha nguo kuonekana ya kuvutia hata kama nguo ni ya kawaida kabisa. Skafu zipo za aina nyingi kama pashmina(mitandio), ndefu nyembamba, za mraba n.k.


Uvaaji wa Skafu


Skafu inaweza kuvaliwa katika mitindo mbalimbali kutokana na umbo lake na mvaaji anataka kuivaa vipi. Skafu inaweza kuvaliwa shingoni, kiunoni kama mkanda au kichwani kama kibanio au kufunika nywele. Skafu kubwa kama pashmina unaweza uitumia kujifunika hasa wakati wa baridi.


Ufungaji wa skafu shingoni


Skafu yenye umbo la mraba unaweza kuikunja kupata pembetatu kisha ukafunga pembe mbili nyuma ya shingo ili ule upande mpana uwe umelala kifuani chini ya shingo.
2.Skafu ndefu nyembamba inavaliwa kwa kuining’iniza shingoni na kuifunga na pini kwa mbele.Unaweza tumia ‘brooch’ au pete maalumu.


3.Skafu ndefu pia unaweza kuivaa shingoni upande mmoja ukining’inia kwa mbele na mwingine ukining’inia kwa nyuma.
4.Pashmina skafu unaweza kuivaa kwa kuikunja nusu na kuiweka shingoni kisha kuchukua upande mmoja na kuuweka ndani ya upande mwingine kama unafunga kamba.