O1, SEPT 2014
Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile
viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya
aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na mavazi
yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu na wapi hasa na
vipi vikitumika vinapendeza zaidi.
1.Viatu vya ngozi vya kufunika
Viatu vya kufunika vipo virefu sana, vyenye urefu wa
wastani na vifupi kabisa. Mara nyingine haviwi vya ngozi kabisa bali ni kama
vina plastiki na pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele.Viatu virefu zaidi
mara hupendeza zaidi kuvaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini
kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na
kupunguza ufanisi.
Viatu vyenye urefu wa wastani unaweza kuvaa popote iwe
kazini, kanisani, kwenye sherehe n.k. Viatu vya chini kabisa vinakuwa vyenye
matumizi zaidi wakati unamatembezi mengi. Havifai sana kuvaa kwenye sherehe za
usiku hasa kama unavaa nguo maalumu ya usiku. Vinafaa sana kwa mjamzito hasa
katika miezi ya mwisho.
2.Viatu vya wazi virefu
Viatu hivi vipo vya aina mbili, vyenye rangi za mng’ao na
ambavyo ni mahususi kwa sherehe za usiku na vyenye rangi ngumu ambavyo waweza
kuvaa kazini au kanisani. Viatu hivi vinapendeza kuvaliwa na nguo yoyote ila
ikiwa ya urefu wa wastani ni nzuri zaidi maana huwezesha kuonekana urembo na
uzuri wote wa kiatu. Viatu hivi vinakuja katika mitindo mbalimbali na unachagua
ule ambao wewe unaupendelea zaidi mfano vyenye visigino vyembamba, visigino
vinene au aina ya ‘wedges’.
3.Viatu vya wazi vifupi
Viatu hivi ni vizuri sababu vinawezesha miguu kupumua na
ku’relax’. Viatu hivi vipo vya aina tofauti tofauti na vinafaa sana kuvaliwa
kwa matembezi ya jioni, wakati wa safari ndefu, wakati ukiwa na mizunguko mingi
na pia hata kazini au kanisani pale unapokuwa umevaa nguo za kawaida (casual).
Havivutii sana kuvaliwa na suti au nguo ya usiku. Pia mara nyingi viatu vya
chini hupendezea kuvaliwa na nguo ndefu( hasa casual) na viatu virefu hupendeza
zaidi kwa nguo yenye urefu wa wastani.
4.Viatu vya muda maalumu
Hivi ni viatu ambavyo vinavaliwa wakati wa kazi maalumu
kama wakati wa kazi za mashambani, mgodini, wakati wa michezo au wakati wa
baridi kali.
Ni vyema na inapendeza kama unauwezo uwe na viatu
vya aina mbalimbali angalau aina tatu. Mfano viatu vyeusi vya urefu wa wastani,
viatu vya usiku vya wazi, viatu vya chini vya kufunika na vya wazi.
No comments:
Post a Comment