Monday 1 September 2014

UREMBO WA MIKONO YAKO KATIKAKUIWEKA SAFI


September 01, 2014 

Posted by Josee Santana-Designer and Model


Description: https://womenofchrist.files.wordpress.com/2010/09/manicure.jpg?w=225&h=300

Mikono ni mojawapo ya sehemu muhimu katika mwili wa mwanamke. Mikono hutumika kufanya shughuli zote za nyumbani kuanzia kupika, usafi, malezi n.k na isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika na kupoteza mvuto wake wa asili. Urembo wa mikono sio lazima ufanyike saluni au kwa wataalamu, wewe mwenyewe unaweza kufanya hivyo kwa muda wako kwa gharama nafuu.

  • Vitu Vinavyohitajika
  • Pamba ya kutolea rangi kama umepaka rangi
  • Dawa ya kutolea rangi
  • Mashine ya kukatia kucha au mkasi mdogo
  • Tupa ya kucha (Nail file)
  • Brash ndogo ya mikono
  • Sabuni ya kunawia
  • Rangi ya kucha kama utapendelea

 

  • Kwa kutumia pamba na dawa ya kutolea rangi toa rangi yote kwenye kucha na hakikisha imetoka kabisa.
  •  
  • Kata kucha zako kwa urefu unaoutaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo.
  • Lainisha ncha za kucha zako kwa kutumia tupa ya kucha, hakikisha unazisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha kuvunjia. Kusugua kwa kwenda mbele na nyuma husababisha kucha kuvunjika upesi.
  • Kwa kutumia maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono, osha mikono yako vizuri na kuisugua  hasa sehemu za kucha.
  • Kausha mikono yako vizuri kisha paka losheni, hakikisha umepaka hadi kati kati ya vidole
  • Kama utahitaji kupaka rangi, chukua pamba na remover na kutoa mafuta kwenye kucha zako kisha anza kwa kupaka rangi ya maji mpako mmoja na ikisha kauka ndipo upake rangi uliyoikusudia. Paka mpako wa kwanza acha ikauke kisha paka mpako wa pili na ukishakauka malizia na rangi ya maji ili kung’arisha na kuleta mvuto zaidi.

Tip: Kama kucha zako zimebadilika rangi kutokana na kupaka rangi mara kwa mara, loweka mikono yako kwenye maji yenye limao kwa dakika 5.

Kama hauna tupa ya kucha unaweza kutumia kiberiti ule upande wenye baruti.

Karibu katika ulimwengu wa urembo kina Dada

 

No comments:

Post a Comment