Saturday 30 June 2012

CHANGAMOTO KATIKA SANAA YA UBUNIFU WA MAVAZI NA MITINDO




Mbunifu wa mavazi na mwana mitindo chipukizi aliyejibebea sifa na umaarufu baada ya kushinda shindano la sanaa ya ubunifu wa mavazi na mitindo lililojulikana kwa jina la Uni Fashion Bash Lake Zone na kuwa moja kati ya mabalozi wa kinywaji cha Reds kinachozalishwa na kampuni ya TBL jijini Mwanza bwana Joseph Simon, ameibuka na kuzungumzia changamoto zinazowakabili wabunifu wanaochipukia katika sanaa nzima ya ubunifu wa mavazi.
Mbunifu huyo alisema kutokana na changamoto nyingi zinazowakabili wabunifu wanaochipukia katika tasnia hii ya urembo na mitindo wmejikuta wakishindwa kuendeleza vipaji vyao walivyonavyo vya sanaa ya ubunifu wa mavazi na mitindo,alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kukosa ufadhili,kutokuwa na pesa za kutoha katika kufanya manunuzi ya matilio yatakayoweza kutengeneza mavazi yao,kukosa masoko ya nguo zao na kutengeneza nguo za kiasili zaidi kutokana na kutokuwa na uwezo. Ata hivyo mbunifu huyo aliomba wanamitindo na wabunifu wakubwa ambao wamejibebea umaarufu mkubwa na kujibebea sifa kemkem katika sanaa hii ya mavazi kama Ali Rymntullah, Mustafa Assanali, Hadija Mwanamboka na wengineo wengi waweze kuwasaidia chipukizi ili kuweza kupata wabunifu wakubwa wa baadae wenye vipaji katika tasnia hii, aliendelea kwa kusema kwamba Swahili fashion ni moja kati ya msaada mkubwa kwa wabunifu wa chipukizi wa sanaa hii ya ubunifu wa mavazi na sanaa ya maonyesho ya mavazi lakini pia aliwaomba wabunifu wakubwa kuweza kuanzisha programu kama hizi katika kuendeleza sanaa hii ya mitindo ya mavazi na maonyesho zaidi