Sunday 23 June 2013

2013



MAONYESHO 5 BORA YA MITINDO YALIYOFANYA VEMA BARANI AFRICA




Muongo uliopita ulishuhudia kukua kwa tasnia ya mitindo na ubunifu barani Afrika. Kile kinachofanywa na tasnia hiyo barani humu kimejaribu kupata mafanikio katika kipindi cha miaka michache iliyopita, ni kuliuza bara hili katika ulimwengu mwingine wa mitindo hasa katika bara Ulaya na Marekani ambao wanaheshimu mitindo ya Africa na kuanza kuwatupia macho wanamitindo wake.
Siku hizi, wabunifu wa Africa wamekuwa wakimiliki brand kubwa, pia wakijaribu kupambana kupata heshima katika maoensho kadha ya Milan na New York, na Paris. Ukuaji huu umekuja baada ya kuwa na utaratibu wa kuwa matukio mbalimbali ya mavazi kama vile wiki za maonesho ya mavazi, ambayo yamezidi kunogesha nafasi ya bara hili katika ukuaji wa mitindo na ubunifu.
Majiji kama vile Johannesburg, Lagos, Accra, na Dakar hufanya maonesho mbalimbali ya mitindo, wakianzisha nyumba za maonesho na rajabu.
Mtandao wa howzitMSN umeangazia 5 bora ya wiki za maonesho ya mavazi ambazo zimekuwa zikijipatia umaarufu mwaka hadi mwaka.
Maonesho ya Mercedes Benz Johannesburg – MBFW Johannesburg – Afrika Kusini
Hii ni sehemu ya Maonesho ya mavazi ya Kimataifa ya Afrika (African Fashion International – AFI) ambayo ina maonesho matatu ikijumuisha, Mercedes Benz Fashion Week – Cape Town na Mercedes Benz Fashion Week Africa, MBFW Johannesburg ni moja ya maonesho maarufu ya mavazi barani Africa.
Maonesho haya hufananishwa nay ale yanayofanyika katika miji ya New York, Madrid na Stockholm. Hufanyika mara moja kwa mwaka hasa katika mwezi wa March.
Maonesho ya Dakar – Senegal
Huenda ikawa ndiyo maonesho makubwa na bora zaidi katika ukanda wan chi za Afrika Magharibi. Maonesho haya yameanzishwa na mbunifu anayeishi nchini Marekani katika jiji la Los Angeles, Adama Ndiaye mwaka 2002.
Kwa muongo mmoja sasa maonesho haya ya Dakar yamekuwa yakiwaweka pamoja wanamitindo na wabunifu mbalimbali kutoka barani Afrika.
Wabunifu wengi, wanaojulikana na wasiojulikana ambao wamewahi kuhudhuria onesho moja ama lingine, huyaelezea maonesho hayo. Na licha ya kuwa na changamoto zake ambazo hujumuisha kukosa uungwji mkono na serikali ya Senegal, lakini yanuwa bora kila mwaka.
Maonesho ya ARISE Magazine – AMFW - Nigeria
Maonesho ya AMFW yamekuwa yakifanyika tangu mwezi March mwaka 2011. ingawa, kutokana na kile waandaaji wake wanachotaja kuwa ni changamoto ya kukosa hati ya kusafiria kwa wabunifu, na kodi inayohusishwa na maafisa wa idara ya uhamiaji, onesho hili haliwezi kuendelea.
Katika miaka michache iliyopita, imekuwa ikiwajumuisha wabunifu wengi maarufu, hasa wale wenye asili ya Africa, na wanaoishi nje ya bara hili.
Waandaaji wamefanya mambo kuwa rahisi kwa wabunifu wanaohama kila mwaka, kuchukua nafasi ya kushindana katika maonesho kama vile yale ya New York na Johannesburg.
Maonesho haya ya AMWF ni uzao wa jarida maarufu la mitindo linalouzwa katika nchi zaidi ya 20 lijulikanalo kama ARISE Magazine.
Maonesho ya Afrika Kusini – SA Fashion Week – Afrika Kusini
Licha ya kukumbana na upinzani mkali kutoka kwa maoensho mengine ya ndani yanayojulikana, maonesho haya ya SA Fashion Week yanaendelea kukua. Tangu mwaka 1996, yamekuwa ni tukio lenye kuhudhuriwa huku yakiwa na lengo la kutafuta kile kiijulikanacho kama “maendeleo ya kiuchumi ya tasnia ya ubunifu na kuwahasisha wateja wa Afrika Kusini kununua bidhaa zitokanazo na wabunifu wa ndani.”
Upinzani huo umezidi kunogeshwa na hoja ya kuvutia siyo wabunifu wa ndani ya nchi hiyo tu, bali hata wabunifu wan je ya nchi. Yanafanyika jijini Johannesburg mara mbili kwa mwaka.
Maonesho ya mitindo na ubunifu ya Lagos – LFDW - Nigeria

Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka wa pili kufanyika maonesho hayo. Yamefanikiwa sana huku yakifuata mafanikio ya mwaka 2011.
Maonesho ya LFDW yanawavutia wabunifu walioanzisha na wale wanaochipukia. “Lengo ni kuenea kupita mipaka yote ya kijiografia na kitamaduni na kuiweka yenyewe kama tukio la kibiashara ya mitindo na ubunifu na kuwa bora katika tasnia ya mitindo na ubunifu, kuongoza tasnia ya mitindo nchini Nigeria na kuimarisha uchumi.”